Office Address
Katusyo
Email Address
info@tukuyu.co.tz
Drop a Line
+255 622 550 011

Historia Ya Tukuyu

Image
Historia ya mji wa tukuyu

Je Wajua Jina Tukuyu Limepatikana Wapi?

Hapa Tanzania kuna sehemu ukienda na ukapewa historia zake unaweza kubaki mdomo wazi, kwa kuwa ukiangalia mji huo kama hauendani na hiyo historia. Lakini kimsingi kuna miji hapa Tanzania kwa kweli imabarikiwa kuwa na historia ya kusisimua. Moja ya mji huo ni Tukuyu.

Tukuyu ni moja ya mji unaopatikana wilayani Rungwe, takrbani kuna umbali wa kilomita 68 kutoka Mbeya Mjini, kilomit 67 kutoka wilaya ya Kyela, kilomita 632 kutoka makao makuu ya nchi yaani Dodoma, kilomita 468 kutoka Songea na kuna umbali wa kilomita 858kutoka mji mkuu wa kibaishara Dar es Salaam.

Ukiwa hapo Tukuyu unaweza kufika maeneo kama Bagamoyo na Tukuyu Stendi. Hali ya hewa katika eneo hili ni baridi sana ukizingatia Tukuyu ni moja ya sehemu inayopatoka nyanda za juu kusini. Kwa wakati wote mji wa Tukuyu unakuwa wa kijina na hii ni kutokana na uwepo wa mvua.

Wakazi asilia wa mji huu wa Tukuyu ni Wanyakyusa waliopata kufika hapo miaka mingi sana hata kabla ya 1800 wakitokea huko Malawi. Ambapo huko Malawi wanafahamika kwa jina la Wakhonde kutoka mkoa wa kaskazini mwa nchi ya Malawi. Lakini kuanzia miaka ya 1900 hapo Tukuyu kulikuwana ujio wa makabila mengine yaliopata kutokea sehemu mbalimbali. Wengi walikuja kwa sababu za kisiasa hasa uwepo wa wakoloni wa kijerumani tangu 1885 na hawa walitokahuko Pwani, yaani Bagamoyo, Pangani na Tanga, na pia uwepo wa biashara hapa nawazungumzia wakazi kutoka Makete, yaani Wakinga.

Karibu Mji wa Tukuyu Upate historia na kuona Maajbu ya mji huu

Jifunze zaidi
Features Image

Ukija upande wa utalii kuna mambo kibao ya kuvutiwa. Kwanza ukiwa unaingia Tukuyu mjini hapo mwanzoni utakutana na mtaa au eneo lianitwa Bagamoyo, hapo utapata kujua historia adimu sana ya wakazi wa mtaani huo. Lakini pia kuna milima ambayo inapatikana Kaskazini-mashariki na kusini Mashariki mwa mji wa Tuyuku, hasa ule mlima Rungwe ambao ni moja ya mlima wa Volkano iliokufa. Ukienda mbele maeneo ya Masoko unaweza kuona ziwa Kisibha au Kisiba ambalo lipo kwenye mlima na lina maajabu kibao ukipata kufika hapo.


Lakini pia hapo Tukuyu kuna shule ya pili kupata kujengwa na serikali ya mkoloni yaani mwaka 1919. Ifahamike kuwa shule ya kwanza ilijengwa huko Tanga na hivyo shule ya pili ilijengwa hapa Tukuyu. Na sababu ya kujengwa shule hiyo ni kutokana na Wanyakyusa kuonekna kupenda Elimu na kuukubari Ukristo kwa haraka sana. Huyo shule inaitwa shule ya msingi Tukuyu na ipo karibu sana na stendi ya mabasi hapo Tukuyu umbali wa mita 10 kutoka hapo Kituo,ukiwa kam unaenda Kyela au mlango wa kuingilia stendi.


Ukiachilia mbali shule hiyo, hapoTukuyu kuna Boma ambalo kwa sasa linatumika na serikali,boma hilo ni la Wajerumani, ambalo lilijengwa baada ya kuzama kwa boma la kwanza kwenye ziwa Malawi(zamani Nyasa) boma hilo ambalo lilijengwa miaka ya 1900 lilitumiwa na wajerumani mpaka walipoondoka miaka ya 1919. Ukiwa hapo Tukuyu boma hilo lipo karibu na Benki ya NMB umbaliwa mita kama 40. Kwa ujumla ukiwa hapoTukuyu utafurahia mengi sana hasa wale wapenda nyama choma na ndizi za kukaanga hapa ndio penyewe.


Asili ya jina Tukuyu, inasimuliwa kuwa mji wa tukuyu ukipata kuwepo hata kabla ya miaka ya 1800. kwani hata hiko kipindi ambacho Wajerumani wanafika miaka ya 1885, waliwakuta wakazi wa hapo ambao ni Wanyakyusa. Lakini kwa kuwa eneo hili lilikuwa na muonekano mzuri, iliwafanya Wajerumani kuweka makazi yao hapo na hasa pale waliopoamua kujengwa lile boma. Na hivyo idadi ya watu kuongezeka siku baada ya siku kutokanana uwepo wa Wajerumani hao ambao nao waliwaleta watu wengi kwa shughuri za kisisasa na kiuchumi.


Na inasimuliwa kuwa zamani kabisa mji wa Tukuyu ulikuwepo ambapo sasa hivi panaitwa Bagamoyo. Kwa kuwa Wajerumani waliwaleta watu wengi hapo na ndipo watu hao walipoanzisha makazi yao na mtaa wao au eneo lao likaitwa Bagamoyo. Lakini kabla ya hapo kulishakuwa na makazi ya Wanyakyusa ambao kisingi hata neno Tukuyu linaanzia huko. Inasimuluwa kuwa neno hili Tukuyu lilitokana na aina ya miti ilioitwa Mikuyu. Na kutokana na maandiko ya wapelelzi wa mwanzo na mchanganyiko wa watu mbalimbali ndipo kukatokea neno Tukuyu na hata kwenye maandiko ya awali palifahamka kama Tukuyu. Na mpaka leo panaitwa Tukuyu.


Kwa ujumla Tukuyu ni mji ambao kwa sasa unakuwa sana na hii ni kutokana na uwepo wamiundo mbinu bora hasa barabara. Ambapo ilipelekea kukua kwa viwanda, na mfano mzuri ni kile Kiwanda cha Maji, na kiwanda cha Gesi. Ukipata nafasi ya kufika hapo Tukuyu utajionea mengi zaidi. Hii ndio habari na historia ya mji wa Tukuyu. Lakini ikumbukwe kuwa, maandiko haya ni sehemu tu ya historia ya Mji wa Tukuyu. Hivyo mawazo yako yanahitajika sana katikakujenga historia hii.