Hapa Tanzania kuna sehemu ukienda na ukapewa historia zake unaweza kubaki mdomo wazi, kwa kuwa ukiangalia mji huo kama hauendani na hiyo historia. Lakini kimsingi kuna miji hapa Tanzania kwa kweli imabarikiwa kuwa na historia ya kusisimua. Moja ya mji huo ni Tukuyu.


Tukuyu ni moja ya mji unaopatikana wilayani Rungwe, takrbani kuna umbali wa kilomita 68 kutoka Mbeya Mjini, kilomit 67 kutoka wilaya ya Kyela, kilomita 632 kutoka makao makuu ya nchi yaani Dodoma, kilomita 468 kutoka Songea na kuna umbali wa kilomita 858kutoka mji mkuu wa kibaishara Dar es Salaam.
Ukiwa hapo Tukuyu unaweza kufika maeneo kama Bagamoyo na Tukuyu Stendi. Hali ya hewa katika eneo hili ni baridi sana ukizingatia Tukuyu ni moja ya sehemu inayopatoka nyanda za juu kusini. Kwa wakati wote mji wa Tukuyu unakuwa wa kijina na hii ni kutokana na uwepo wa mvua.
Wakazi asilia wa mji huu wa Tukuyu ni Wanyakyusa waliopata kufika hapo miaka mingi sana hata kabla ya 1800 wakitokea huko Malawi. Ambapo huko Malawi wanafahamika kwa jina la Wakhonde kutoka mkoa wa kaskazini mwa nchi ya Malawi. Lakini kuanzia miaka ya 1900 hapo Tukuyu kulikuwana ujio wa makabila mengine yaliopata kutokea sehemu mbalimbali. Wengi walikuja kwa sababu za kisiasa hasa uwepo wa wakoloni wa kijerumani tangu 1885 na hawa walitokahuko Pwani, yaani Bagamoyo, Pangani na Tanga, na pia uwepo wa biashara hapa nawazungumzia wakazi kutoka Makete, yaani Wakinga.
View More